TANGAZO 1
” Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda.
Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga,
lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati. Alimtafutia
kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua
akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba.
Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa…hivyo
akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake.
Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo…
Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza
wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake..
Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema
siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo
mpenzi wanafsi yake.
Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika
watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho… Hivyo
wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada
ya yule msichana kumsifia sana.
Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani
ya mfuko.. mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!!
Lahaula… watu wote wakastaajabu..mkate??? Lakini kabla hajasema
lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanzakulia.. akapandwa hasira
kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!! Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida
shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate
na kuutupa.!!
Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi
high table na kusema “baby nakushukuru kwa yote.. Huenda umenidharau kwa
kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii.
Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya..”
Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoaufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday.
Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema “Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote.
Nilipanga
leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa…. Lakini kwa
kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya
thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu
bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe,
nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza..”
Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late..
UJUMBE..!
Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu
ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na
si rahisi kuonekana.. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la
nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua
haukua mkate wa kawaida… kuna vingi vya thamani ndani yako.
Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!!
TUELIMISHANE MEMA…
Imetolewa kutoka mitandao ya kijamii.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3

Post a Comment