TANGAZO 1
VITENDO
vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa
vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za
wanawake na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi
nchini.
Msichana
wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo) anayesoma shule
moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na kadhia ya kuvuliwa
nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi na walimu wanne
wa shule hiyo.
Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha Polisi Mbalizi wilaya ya Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba MBI/IR/967/2016 na kuwekwa kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016 linadaiwa kuwahusisha walimu wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu watatu.
Akizungumza
huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi ambako
amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa na
mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa
pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga
na mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.
Alisema
walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku akiwa
amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la
Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.
‘’Wakati
naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza kunishika
huku chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana miguu
wakazidi kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’alisema mwanafunzi huyo.
Alisema
sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja
alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo
zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.
Anafafanua
kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa na
walimu wanne hadi alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na
kujificha.
‘’Niliwaponyoka
walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule nikajificha hadi
jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada walinichukua
na kunileta hospitali,’’alisema.
Mwandishi
wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia ya
kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.
‘’Mie sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu ya taarifa mnazohitaji,’’alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.
Kwa
upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa adhabu
aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu za
adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa viboko
vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.
‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu,’’alisema Mwakalila.
Naye
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa juu
ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye
yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na
kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.
Awali
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika
Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia
mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu zake
za makalio na kwenye mapaja.
Mtunguja
alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama ambacho
hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha walimu
hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu.
Muuguzi
Mkuu Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga alisema kuwa
mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 21 saa 7:00 mchana
ambapo alipatiwa matibabu na kulazwa kutokana na majeraha na damu
iliyovilia mwilini sehemu za makalio na mapaja.
‘’Ameshambuliwa
sehemu za mapaja, damu na masikio yake hasikii vyema kutokana na
kipigo, anaendelea na matitabu hapa hospitali,’’alisema Sanga.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment