TANGAZO 1
MARA nyingi vijana hupata taabu sana katika suala la kuchagua mchumba.
Vijana wa kiume ndio hasa hupata wakati mgumu zaidi kwani jamii imewapa
wajibu wa kuanzisha mazungumzo yahusianayo na mapenzi.
Hata hivyo, vijana wa kike nao wanao wajibu wa kuchagua ili kuhakikisha
kuwa hawaanguki mikononi mwa mabazazi wa kuwalaghai na kuwatumia kwa
raha za miili yao kisha kuwaacha kwenye mataa.Ni jambo la kawaida kwa
vijana walio wengi, wawe wa kike au wa kiume, kuangalia sura na
mwonekano wa mtu.
Lakini unapotafuta mchum ba kwa malengo ya kuishi naye maisha yako yote
kama mume na mke haipendezi kuangalia tu mwonekano, maana Waswahili
husema si kila king’aacho ni almasi. Kwa sababu hiyo, hapa yatabainishwa
mambo muhimu ya kuangalia na kuzingatia katika suala hili.
1. UADILIFU Pamoja na sifa zote za uzuri zinazoweza kubainishwa na
kufanywa kuwa vigezo vya uzuri wa mwanamke na mwanaume na hata
zikatumiwa kumpata Miss au Mr Tanzania, sifa kuu impasayo mtu anayefaa
kuwa mchumba kuwa nayo ni sifa ya uadilifu.
Mtu anapokuwa na uadilifu (pengine uaminifu), maana yake ni kwamba tabia
ya mtu huyu anayoionesha nje ndiyo tabia yake halisi na anapofanya
jambo jema analifanya kwa roho yake na si kwa unafiki.Mtu anapokuwa
mwadilifu ataheshimu maadili na kufanya wema, hata pale inapokuwa rahisi
kwa wengine kukengeuka na kufuata njia za mkato ambazo mara nyingi si
za halali.Mtu mwadilifu pia huwa na sifa za ukweli na kujitolea
kuwasaidia watu wengine bila kujali faida – haya yote ni mambo muhimu
ambayo mtu mwenye kuwa nayo huwa na msingi wa ujenzi wa uhusiano imara
na wa kudumu.Watu wanaoweza kujivunia furaha ya kweli katika maisha yao
ya ndoa, ni watu ambao wamekutana wote wakiwa na sifa ya uadilifu ambayo
hujumuisha mambo mengi.
Zipo ndoa nyingi zenye furaha ya bandia. Furaha hii mara nyingi hutokana
na ridhiko la kimwili alipatalo mtu kutokana na kukidhiwa kwa mahitaji
yake ya kimwili yanayohusiana na haki za msingi za binadamu – yaani
chakula, mavazi na malazi. Lakini furaha ya kweli ya maisha ya ndoa,
watu hawaipati isipokuwa katika uhusiano ambao wenza wamethibitishana
kuwa waadilifu.
2. HEKIMA, Mtu mwenye uadilifu wa kweli, mbali na kuwa mwema kwa
mwenzake, pia huhakikisha anakabiliana kwa busara na hekima na matatizo
yote yanayoweza kusababisha kuyumba kwa uhusiano, hususan yale yaliyo
nje ya uwezo wake.Uzoefu unaonesha kuwa wapenzi, hususan wanandoa walio
katika uhusiano wa muda mrefu wanaoendelea kufurahia unyumba wao si wale
ambao walipendana kwa mvuto na wala hawana mambo mengi ya asili
yanayowaunganisha kuliko wale wanaotengana.
Lakini la muhimu ni kwamba watu hawa huwa wamejifunza jinsi ya
kukabiliana kwa hekima na matatizo yanayojitokeza, hususan yale
yanayotokana na tofauti zao kimtazamo.Ukiachilia mbali sifa ya uadilifu,
watu hawa huwa wamejifunza kukabiliana na matatizo kuhusiana na uzazi
na ulezi wa watoto, uhusiano na ndugu, jamaa na marafiki, suala la
ngono, fedha na maisha ya unyumba kwa ujumla.Habari njema ni kwamba
uadilifu na hekima ni mambo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza na kisha
kufanyia kazi.
Ndiyo maana wanandoa hufundishwa kabla ya ndoa na hata wanapokuwa tayari
wameoana huendelea kuhudhuria semina za kidini na kijamii kwa ajili ya
kujiimarisha.Kwa hiyo, kama mume/mke wako mtarajiwa anaonekana kuwa na
utayari wa kujifunza kuhusiana na jinsi ya kuishi na mtu wa jinsia
nyingine, ana nafasi kubwa ya kuwa mke/mume mzuri baadaye.
3. UPOLE, Mfalme Suleiman katika mojawapo ya semi zake za hekima alisema
mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake. Yamkini ndivyo
ilivyo pia kwa mwanaume mpumbavu, maana upumbavu haujengi.Siku zote kitu
kinachovunja uhusiano wa kindoa si makombora ya nyuklia, bali ni ulimi.
Kwa kadri mtu anavyoutumia ulimi wake anaweza kuijenga au kuibomoa
nyumba yake.Katika kumwangalia mtu ambaye unaweza kujenga naye nyumba ya
kudumu, ni vema kumchunguza na kuhakikisha kuwa si mtu mwenye kupenda
kurefusha maneno, maana hakika huyu atasababisha ugomvi mara kwa mara na
uhusiano hautadumu.
Wapo watu ambao ndoa zao zina sifa ya ugomvi na karibu kila mtu
anafahamu na hata wamekuwa kero kwa ndugu, jamaa na majirani zao, mara
kwa mara wakiwaamsha watu usiku wa manane wakitafuta suluhu.Mara nyingi
wanaume ndio huanzisha ugomvi, lakini ugomvi huwa na nguvu zaidi kama
mwanamke ni msemaji. Dawa ya kuzuia ugomvi usiokuwa na mpango ni
kupunguza maneno na kuepuka kutafuta ushindi katika ubishi. Lakini kinga
ya tatizo hili ni kuepuka kujiingiza katika uhusiano na mtu ambaye
umejihakikishia kuwa si mwingi wa maneno.
Bahati nzuri, jamii huwatambua wanawake/wanaume ambao wanaweza kuwa
wake/waume bora baadaye kwa hiyo ni wajibu wa mtafutaji kuhakikisha kuwa
anafanya uchunguzi wa kina kabla ya kujitosa kwa mtu ambaye baadaye
atamtaabisha.Mwanandoa aliyeifahamu vema dhana ya ndoa – kwamba ni
maisha ya kuvumiliana na kuchukuliana, hufahamu ni wakati gani wa kusema
na wakati gani wa kukaa kimya.
Mtu huyu pia hufahamu njia nzuri na salama ya kujiondoa kwenye tatizo
anapoona mwenzake anaelekea kubaya, ili hatimaye uhusiano wao uendelee
kuwa salama japo wao wanaweza kuwa wamekwaruzana.Mtu huyu mwenye upole
hujiweka katika mkao wa upatanishi na huhakikisha kuwa kila mjadala
mkali unapita na kumalizika salama. Ni wazi kuwa katika kutafuta, kama
hukukurupuka, utamwona mtu mwenye hulka hii – upole.
4. MVUTO, Hisia za mvuto wa kimapenzi ni muhimu katika kujenga uhusiano.
Mtu mmoja akauliza, ni yupi bora – yule anayenivutia sana au yule
anayenipenda sana? Maisha ni ya ajabu sana. Huwa inatokea kuwa mtu
unayevutiwa naye sana yeye havutiwi nawe, bali anavutiwa na mwingine
ambaye naye hana mpango naye!Haya ndiyo maisha. Uzoefu unaonesha kuwa
asilimia kubwa ya watu walio katika ndoa hawajawaoa/kuolewa na watu
waliokuwa wakiwapenda sana enzi za ujana wao, au wale waliotimiza ndoto
za ujana wao. Bahati njema miongoni mwa wanandoa hawa wapo wale wenye
ndoa imara sana.
Mvuto wa kimapenzi ni muhimu sana, lakini watu husema maji yakisema
usininywe yajibu kuwa wewe pia huna kiu nayo. Japo inaweza kuonekana
kama ni aina ya ‘sizitaki mbichi hizi’ lakini si vema kujisumbua na mtu
asiyekupenda.Badala ya kujihangaisha na mtu asiyekupenda, kaa chini na
umsubiri anayekupenda hata kama huhisi kuvutiwa naye sana.
Baadaye utamzoea na maisha yatakuwa mazuri, kisha utajiuliza baadaye
yule aliyekuringia alikuwa na nini cha ziada?Lakini iwapo mambo mengine
yote yatakwenda sawa, ni vema na muhimu kabisa kuhakikisha kuwa mtu
unayepanga kuwa naye maisha yako yote ni mtu anayekuvutia kimwili na
kiakili, maana vinginevyo unaweza kupata sababu ya kukidhi kiu yako nje –
jambo ambalo si maadili mema katika ndoa na maisha.NI MUHIMU KUWA
MAKINIKatika nyakati za ujana, watu wengi hubabaishwa kwa mengi.
Vijana wa kiume hubabaishwa na sura, maumbile na pengine rangi na
kusahau mambo muhimu yaundayo orodha ya sifa za mke mwema.Kwa upande
wao, vijana wa kile pia waweza kubabaishwa na pesa, maumbile, sura,
utanashati, umaarufu au kuchoshwa na shinikizo la umri, hivyo kujikuta
wakijitumbukiza kwa wanaume wasio na sifa za waume wazuri.Lakini
tukirejea kwenye msemo wa zamani kuwa uzuri si hoja bora tabia, ni wazi
kuwa tutafikia mahali tutajenga mahusiano imara na yasiyotikiswa na
sunami zozote za kimaisha. Ilimradi tu uhakikishe kuwa mtu mwenyewe
anakupa mvuto kimapenzi, maana vinginevyo kutakuwa hakuna maana.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment