TANGAZO 1
HABARI zenu
wapendwa wasomaji wa safu hii. Nimefurahi tumekutana tena kwa mara
nyingine ili kupeana mawili matatu yanayohusu mahaba, hasa kwa kuwa
baada ya kazi ngumu za kujenga taifa letu, tunahitaji nafasi kwa ajili
ya kupumzisha mwili kiakili.
Juzi
nilikuwa na rafiki yangu mmoja tumekaa sehemu tunabadilishana mawazo,
akanipa simulizi ambayo imezaa mada hii. Alinisimulia mkasa wake kuwa
anahisi mke wake anatoka na mtu mwingine, kwa sababu baada ya kuishika
simu yake kwa siri na kuipekua, alikutana na baadhi ya sms zilizompa
utatanishi kidogo, ingawa alishindwa kujiridhisha moja kwa moja kuwa
zilikuwa zinatoka kwa mwanaume.
Baada
ya kukutana na tukio hilo, kwa sababu alishindwa kumuuliza mkewe kwa
hofu ya kuonekana kupekuapekua simu yake, basi alichofanya ni kumkumbuka
mmoja wa michepuko yake kisha akapanga naye kukutana sehemu ili kuondoa
stress.
Hapo
ndipo nilipojikuta nabaki hoi, kwani aliniambia kila mara inapotokea
hali kama hiyo, anachofanya ni kutoka nje ya ndoa yake na akishafanya
hivyo, roho yake hubaki kwatu. Sababu kubwa ya kufanya hivyo, kwa mujibu
wa maelezo yake, eti kama mbwai na iwe mbwai tu.
Ingawa
nilimsikiliza na kumwelewa, lakini sikutaka kumuacha aendelee kuwa na
tabia hiyo, siyo kwa uwezekano wa magonjwa ya zinaa, bali kisaikolojia,
akili yake anaiweka katika sehemu ambayo haimsaidii.
Dawa
ya kupigwa ngumi haiwezi kuwa kurudisha ngumi kwa sababu ugomvi
hautakwisha. Ili kuondoa ngumi, ni lazima kukaa na anayekupiga ili kujua
sababu ya kukupiga, maana huenda unafanya kosa bila wewe kujua kama
unakosea.
Unajaribu
kujiuliza, kama mke atapata hisia za kusalitiwa na mume wake, halafu na
yeye akatoka nje ili kulipa kisasi, hii itakuwa ni ndoa ya aina gani?
Yaani watu hao wawili wakihisiana tu, ndani kumechafuka, kila mmoja
anatoka kumtafuta mbadala!
Hivi
itakuwaje kama ule mchepuko wako nao utakuletea za kuleta, kwa mfano na
wenyewe ukagundua kwamba haujatulia, kwa hasira utakwenda kumtafuta mtu
mwingine wa tatu?
Kama
tunaamini katika mapenzi au ndoa zetu, basi dawa nzuri ya kuhimili
kutendwa, ni kukaa na mwenza wako na kumueleza kwa uwazi kuhusu hisia
zako, kwani hilo ndilo suluhisho la kudumu na tena lililo salama.
Mwambie kuhusu ujumbe mfupi wa maneno ulioukuta katika simu yake, huenda
anaweza kukuondolea hofu yako kwa kutoa ufafanuzi ambao utauelewa.
Watu
wengi walio katika uhusiano au ndoa, hutikisa uhusiano wao kwa sababu
ya hisia tu pasipo ukweli wowote. Ni kwa sababu tu amesikia akiongea na
sauti ya kike au ya kiume, basi moja kwa moja huamua kuamini kuwa
anayezungumza naye ni mpenzi wake.
Nimeshawahi
kusema huko nyuma, kwamba hakuna raha katika uhusiano wa kimapenzi kama
kujifanya kama vile humuoni mwenza wako na wala humfuatilii. Unampenda,
lakini usiruhusu akili yako iumie juu yake. Achana na simu yake, mwache
azungumze kadiri anavyotaka na wala usihoji kuhusu mwanamke au mwanaume
uliyemuona naye.
Anayesaliti
hujitambulisha mwenyewe, kama ni simu, ataenda kuongelea mbali na wewe
ulipo, kama ni ujumbe wa simu, basi atakutazama kwanza kabla ya kujibu
na vitu vingine kama hivi. Unapomtambua kwa dalili hizi, unamuumiza
zaidi kama hutamuuliza kwa sababu hataelewa unachokiwaza moyoni mwako !
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment