TANGAZO 1
Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na
msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa
kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na
funguo nimeshatupa.
Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole
kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea
chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.
Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi
niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni
mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya
leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu
walichezea amani, hata amani inalevya.
Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja,
mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya
chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma
washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata
sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.
Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk
Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu
akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua
Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme,
watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo
la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu
wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu
aliekanyagwa huku.
Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu
wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba
wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa,
tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua
karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi.
Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni
watu wachache sana.
Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku
lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo
anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na
umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha
umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri
sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment