TANGAZO 1
Siku chache tangu m c h e k e s h a j i mwenye jina kubwa Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ auage ukapera kufuatia ndoa yake iliyozua gumzo, nyepesi nyepesi za mjini zinasema kuwa kutoonekana katika shughuli hiyo kwa msanii mwingine, Silvery Mujuni ‘Mpoki’ kunatokana na bifu zito lililopo kati yao, Risasi Mchanganyiko limedokezwa. Mpoki na Vengu walikuwa ndiyo wasanii pekee wa kundi mahiri la vichekesho la Orijino Komedi ambao hawakutokea katika shughuli hiyo ambayo awali ilianzia katika Kanisa la Miito ya Baraka Kariakoo na baadaye katika Ukumbi wa Prime Rose, Mbezi Beach jijini Dar. Inafahamika kuwa Vengu ana matatizo ya kiafya na hajaonekana hadharani kitambo sasa.
KISIKIE
CHANZO Chanzo chetu ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake, kilisema
ilikuwa ni jambo la lazima kwa Mpoki kuwepo katika shughuli hiyo, kwani
alikuwa jijini, lakini kuwepo kwa tofauti kati yao, kulisababisha
mtangazaji huyo wa redio kwa sasa, kutoonekana kwenye harusi na tafrija
ya memba mwenzake huyo, anayetajwa kuwa ndiye mwenye mafanikio zaidi
kuliko wote ndani ya kundi lao. “Mimi nawaambieni Masanja na Mpoki kuna
kitu. Jiulizeni kwa nini waigizaji wengine wa kundi lao walijitokeza
kumsapoti mwenzao kwa kukata mauno kasoro lakini Mpoki hakuhudhuria
wakati alikuwa hapahapa mjini akiendelea na mishemishe zake? Fuatilieni,
kuna kaukweli,” kilisema chanzo hicho.
RISASI
MCHANGANYIKO LAINGIA MZIGONI Kufuatia madai hayo, gazeti hili liliingia
mzigoni kufuatilia ukweli wa jambo hilo na sehemu ya kwanza, ilikuwa ni
kwenye mitandao ya kijamii ambako lilihoji kulikoni Orijino Komedi?
Katika mtandao mmoja maarufu Bongo, wachangiaji mbalimbali nao
walionesha kuhoji sababu za msanii huyo, ambaye pia hujiita Mwarabu wa
Dubai, kutoonekana, wakidai kuwepo kwa matatizo kati yao,
yanayosababishwa na masilahi. “Ishu siyo Masanja na Mpoki ni Mpoki na
Kundi la Orijino Komedi. Kundi linaonekana kama limekufa, hawatoi kazi
mpya, kila mtu anaonekana kufanya kazi kivyake na
hawashirikiani katika shughuli za kijamii kama zamani,” aliandika mchangiaji mmoja katika mtandao huo. Mchangiaji mwingine alisema kuwa tatizo linalotokea ni ukweli kuwa Masanja Mkandamizaji, ambaye ni kinda katika sanaa kuliko Mpoki na Joti, amefanikiwa sana kutoka kimaisha kuliko wenzake, jambo linalowafanya waingiwe na kinyongo. Baada ya mitandao hiyo na kuona maoni hayo ya wachangiaji, gazeti hili liliamua kukata mzizi wa fitina kwa kujaribu kuwafikia wasanii hao ili kupata ukweli wao.
hawashirikiani katika shughuli za kijamii kama zamani,” aliandika mchangiaji mmoja katika mtandao huo. Mchangiaji mwingine alisema kuwa tatizo linalotokea ni ukweli kuwa Masanja Mkandamizaji, ambaye ni kinda katika sanaa kuliko Mpoki na Joti, amefanikiwa sana kutoka kimaisha kuliko wenzake, jambo linalowafanya waingiwe na kinyongo. Baada ya mitandao hiyo na kuona maoni hayo ya wachangiaji, gazeti hili liliamua kukata mzizi wa fitina kwa kujaribu kuwafikia wasanii hao ili kupata ukweli wao.
HUYU
HAPA MASANJA MKANDAMIZAJI “Mimi na Mpoki ni kama ndugu kaka, hakuna
kitu kama hicho, siku ya ndoa yangu alikuwa na mambo yake binafsi, ndiyo
maana hakuweza kutokea, lakini wengine walimuwakilisha, kwa hiyo hizo
tetesi hazina mashiko kabisa,” alifunguka Masanja na kuongeza; “Madai ya
kundi kumomonyoka pia hayana ukweli wowote, Orijino Komedi inaendelea
na kazi zake kama kawaida, napenda kuwaambia tu Watanzania kwenye kundi
letu kulikuwa na mlango wa kuingilia tu na hakuna wa kutokea, kama
mnabisha au mnataka kuamini zaidi basi zungumza na msemaji wa kundi,
Seki,” alisema.
MPOKI
ASAKWA, AKAUSHA Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mpoki kupitia simu yake
ya mkononi, lakini haikupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno,
alikataa kusema lolote, badala yake akajibu; “Namba ya Masanja hiyo
muulize,” alisema huku akitoa namba ya muigizaji mwenzake huyo. SEKI
SASA Kiongozi na msemaji wa kundi hilo, Sekioni David maarufu kama Seki,
alisema kundi lao lipo imara ingawa ni muda mrefu hawajatoa kazi.
“Wasanii wapo mapumziko na tunatumia muda huu ili kuboresha mikataba
yetu ili tutakaporudi, tutakuja na kitu kingine tofauti kabisa.” Kuhusu
kutoonekana kwa Mpoki harusini na kwenye sherehe, msemaji huyo ambaye
pia ni msanii wa kuigiza sauti za watu, alisema; “Kwa nini humuulizi
Vengu, kulikuwa na wawakilishi wake pale mbona huwasemi? Si unafahamu
kama Mpoki pia ni MC? Siku hiyo alikuwa na kazi nyingine ndiyo maana
hakutokea.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment