TANGAZO 1
Kutengeneza
uhusiano wenye nguvu ni moja ya mambo yenye changamoto kubwa. Japo
hakuna maelekezo maalum, kuna mambo machache na rahisi ambayo unaweza
kumwambia mpenzi wako yakaujenga zaidi. Weka desturi ya kusema mambo
haya kwa mpenzi wako na muda mfupi tu mtakuwa couple itakayowapa wivu
marafiki zetu.
1. Nakupenda
Nakupenda
ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mpenzi wako. Hakikisha tu kuwa
unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mpenzi wako
anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko
pamoja.
2.Nilikuwa nakuwaza
Ni
muhimu kumjulisha mpenzi wako kuwa unamuwaza hata kama hamko sehemu
moja. Ukiona kitu kizuri au cha kuchekesha katika siku yako ambacho
kinakufanya umkumbuke, mjulishe.
3. Siku yako ilikuaje?
Muulize
masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku.
Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa
waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za
maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.
4. Nakuunga mkono
Mpe
moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake.
Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo
aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu
mwingine upande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu,
kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha
uhusiano wenu.
5.Umependeza
Picha na OGS Studio
Kama
umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika
mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha
kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na
kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
6. Samahani
Kila
mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno
kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi
kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba
msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako.
Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.
7. Hakuna kama wewe
Mpenzi
wako anatakiwa kuwa rafiki yako. Kama hautaki kutembea naye, basi
hamkupaswa kuwa kwenye uhusiano. Mfanye mpenzi wako ajue kuwa yeye ni
bora na hakuna kama yeye.
8. Napenda mawazo yako
Mwambie mpenzi wako kuwa unapenda mawazo yake. Mjulishe kuwa unaona ana akili, mcheshi, anajua kupenda na ana kipaji.
9.Nakuheshimu
Kama
ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi
wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo
yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na
salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
10. Napingana na hilo
Sehemu
moja wapo ya kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale usipokubaliana
naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila kitu na hakuna
mwanamke anayetaka kuzaa watoto na mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza
kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya
kila mmoja. Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa
mpenzi wako mtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa
tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.
11. Usiku mwema
Tunaishi
kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe
tunaweza kutuma ujumbe kuvuka bahari, hivyo hakuna kisingizio cha
kushindwa kusema ‘usiku’ mwema.
Haimjulishi
mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa
unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana,
maliza siku na kishindo chanya.
Chanzo: Lifehack via bongo5
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment