Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SHILOLE AKIRI KUPENDANA NA STAA WA MUZIKI KUTOKA NCHINI NIGERIA WIZKID

TANGAZO 1
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed Yusuf a.k.a Shilole au Shishi Baby, amekiri kupendana na staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun ‘Wizkid’.


Kauli ya Shilole inakuja kufuatia madai mazito ikisemekana kwamba, alilala na jamaa huyo katika hoteli moja maarufu (jina linahifadhiwa) jijini Mwanza walipokutana kwenye Shoo ya Fiesta. Kabla ya mwanamama huyo kuvunja ukimya juu ya Wizkid, chanzo makini kilichoambatana na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva jijini Mwanza, kilieleza kuwa ishu hiyo ilianzia kwenye Viwanja vya CCM-Kirumba ambako ndiko kulikuwa na shoo hiyo ya Fiesta iliyofanyika wikiendi iliyopita. Ilidaiwa kuwa, Shilole alionekana akiwa beneti na Wizkid huku akigandana naye kama ruba. 
 

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, wawili hao walionekana, wakiwa sambamba kwani hata nyuma ya jukwaa (backstage) walikuwa wakinyweshana vinywaji na kila mmoja akionekana kumzimikia mwenzake. Ilielezwa kwamba, hali hiyo ya ‘kubebishana’ iliendelea hadi kila mmoja alipomaliza kufanya shoo ambapo waliondoka pamoja uwanjani 
WAANDISHI WETU, RISASI hapo kuelekea hotelini. “Habari ya mjini kwa sasa ni Shilole na Wizkid kwani kuanzia mwanzo wa shoo walikuwa pamoja mpaka mwishoni kabisa waliondoka pamoja. Kiukweli ndani ya muda mfupi walionekana kuzimikiana sana huku wakinyweshana vinywaji na kubadilishana mawasiliano nyuma ya jukwaa,” kiliendelea kudai chanzo hicho. 

WAZUA MINONG’ONO 

Chanzo hicho kilieleza kuwa, ukaribu wa mastaa hao ulizua minong’ono kwa mashabiki huku wengine wakiufurahia na baadhi kusema kuwa, mastaa wa kike wamezoea kujirahisisha kwa wanaume mastaa wakubwa wakidanganyika na umaarufu au fedha. “Hawa wasanii wa kike wana matatizo sana, maana wakimuona mtu maarufu au mwenye fedha, wanawashobokea sana. Yaani wanajikuta wanajirahisisha mno kitu ambacho kinawashushia hadhi na kuonekana hawana thamani kabisa. “Hebu angalia Shilole alivyochanganyikiwa, kisa Wizkid,” alisikika shabiki mmoja akiwaambia wenzake.

SHILOLE AKIRI KUPENDANA NA WIZKID 

Baada ya kunyetishiwa lilimsaka Shilole na kummwagia mashitaka yake yote ambapo alikiri kupendana na Wizkid: “Kiukweli hakuna mwanamuziki ambaye nimempenda kama Wizkid na yeye amenipenda na kunikubali sana maana wanamuziki wengine tuliokuwa nao, waliniambia kwamba jamaa amenikubali sana. “Kuonesha kwamba Wizkid alinikubali amenifollow Instagram na kule Mwanza tulibadilishana mawasiliano na tunaendelea kuwasiliana. Hilo la kulala pamoja au kumpa penzi bado hatujalifikia jamani,” alisema Shilole ambaye kwa sasa ni mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva ambaye ni zao la THT, Hamad Hassan ‘Hamadai’.

HUYU HAPA HAMADAI 

Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilimfikishia Hamadai ubuyu huo ili kusikia upande wake ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Mimi nilikuwa Mwanza na nilishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na ni kweli Shishi alikuwa karibu na Wizkid. “Hilo la kulala pamoja naomba nikuhakikishie kwamba siyo kweli na ni maneno ya watu tu, mimi ndiye nililala naye (Shilole) na tupo freshi kabisa hakuna tatizo.”
TUJIKUMBUSHE Mapema Februari, mwaka huu, mwanamuziki mwingine wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ alidaiwa kubanjuka na mwanamuziki Wizkid alipotinga Dar kwenye shoo na kulala naye katika hoteli moja iliyopo Masaki jijini Dar. 

Waandishi: Gladness Mallya na Imelda Mtema.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright SUKARI GURU
Back To Top