Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Polisi matatani kwa kumjeruhi raia mwema!

TANGAZO 1


Manyama ambaye ni majeruhi aikifikishwa hospitali

Na Waandishi Wetu, RISASI Mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Baadhi ya askari wa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ wameingia matatani kwa maana ya lawama kufuatia madai ya kumpiga mpaka kumjeruhi mfanyakazi wa Taasisi ya Mikopo ya Wezesha Mzawa, Boniface Manyama yenye makao yake, Sinza Afrikasana jijini Dar na kusababisha kulazwa Hospitali ya Mwananyamala.

Manyama

Kwa mujibu wa meneja wa taasisi hiyo, Samson Luiza, siku ya tukio, Julai 30, mwaka huu ndani ya ofisi zao, mteja mmoja aliyetajwa kwa jina la Sophia Urio akitajwa kuwa chanzo kikuu.

“Ishu iko hivi! Sophia ni mteja wetu kwenye mikopo. Awali alikuja akakopa kiasi cha pesa (hajakitaja). Akarejesha vizuri na kukopa kiasi kingine ambacho ni kikubwa kuliko cha mwanzo.

“Sasa kwenye kurejesha ikawa shida kidogo, na kwa mujibu wa mkataba wetu na yeye, akishindwa kulipa mpaka ngazi ya muda f’lani, kinachofuata ni kuchukua vitu vilivyopo kwenye dhamana na kuvipiga mnada kwa lengo la kurejesha fedha zetu ili wateja wengine waendelee kukopa.”

Sophia Urio

“Ilipofika muda huo, tulifunga safari mpaka Mbezi Kati anakoishi, tukaonana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, anaitwa Alex ambapo tuliweka kikao na mteja wetu, akaahidi kulipa tarehe za mbele. Basi, sisi tukaondoka.

“Lakini ule muda ulipofika hakutimiza ahadi yake. Ikabidi twende tena. Safari hii tulikwenda kwa lengo moja tu, kuchukua vitu. Kwani tuliongozana na mwanasheria wetu anaitwa Godlucky William.”

“Siku hiyo pia tulimkuta mume wa mteja wetu, anaitwa Luke Kimweri ambaye baada ya kujua sababu ya ujio wetu tukiwa na Mjumbe wa Nyumba Kumi, Augustino, aliahidi kulipa yeye deni lile.

“Siku ileile mumewe alilipa shilingi laki mbili keshi. Halafu akaahidi tahere nyingine kupunguza tena. Maana jumla ya deni ilikuwa shilingi 946,888.

“Tuliondoka na kiasi hicho kwa lengo la kusubiri tarehe nyingine aliyosema mumewe. Ilipofika, yule mwanaume alilipa tena kwa kutuma kwa mtandao wa simu ya mwanasheria wetu (kwa sasa ameacha kazi).”

“Naweza kusema yule mume wa Sophia ni mtu mwenye kujali ahadi zake. Alipotuma kiasi hicho tena, aliahidi kumalizia kiasi kilichobaki ambacho ni shilingi 303,500 Julai 29, Ijumaa iliyopita. Na kweli, siku hiyo akatuma kiasi chote hivyo, mteja wetu akawa amemaliza deni lake lote.”

“Sasa kwanza, Ijumaa hiyohiyo, nilikutana na Sophia, akanipa barua. Nikamuuliza ya nini, akasema niisome, yeye akaondoka.

“Niliifungua, iliandikwa kutoka Kituo cha Polisi cha Wazo Hill (Dar). Barua ilisema inamuita bila kukosa kituoni hapo, William. Haikusema William nani? Tena iliandikwa Kwa: William? Yaani ilimalizia na alama ya kuuliza.

“Halafu ikaandikwa anakopatikana William ni Afrikana Mtaa wa Wezesha Mzawa. William alitakiwa kufika kituoni na kuonana na afande Vumilia.

“Mimi pale Mzawa sina William. Nilikuwa na Godlucky William na aliacha kazi kwa amani tu. Kwa hiyo nikajua kuna makosa yamefanyika. Lakini nilimpigia Godlucky nikamweleza.”

“Sasa Jumamosi ya Julai 30, nikiwa ofisini, nikasikia kelele, watu wameingia wakiuliza Manyama ni nani? Wakarudiarudia kuuliza. Nilipoangalia vizuri kupitia upenyo fulani nikawaona askari wakiwa wameongozana na Sophia. Nikashangaa sana.

“Sofia akamnyooshea mkono mtu mwingine akidai ni Manyama. Sasa wakawa wanamtaka Manyama na si William, Lakini ghafla, nikasikia mtiti wa nguvu. Nikasikia Manyama akilalamika kwamba anapigwa kwenye chumba kingine ambacho alikimbilia.”

“Nilipoona vile, nilitoka mbio, nikaingia ndani ya gari na kukimbilia Bamaga (Mwenge) kumweleza mkurugenzi wa taasisi ambaye ni Eric Shigongo. Ikabidi na yeye atoke ofisini na kukimbilia eneo la tukio.”

“Tulipofika eneo la tukio, tulikuta polisi wamemkunja mfanyakazi mwingine wa taasisi wakidai alikuwa anataka kumficha Manyama kwa kuficha funguo ya chumba alichokimbilia. Lakini pia, walimchukua Manyama akiwa anavuja damu kwa kipigo na amepasuka sehemu ya mbele ya paji la uso na wakiwa wamemfunga pingu, wakamwingiza nyuma ya gari, kwenye buti.

“Tuliumia sana. Shigongo akasema… …si sawasawa kumuweka majeruhi kwenye buti. Ni yale magari yao ya sasa, Layland Ashok. Akazuia gari kutoka kwenda Mabatini mpaka majeruhi wetu awekwe siti ya kati. Polisi wakasema wanazuiwa kufanya kazi yao.

“Kha! Jamani, sasa mtu ameumia vile na damu juu, tena wamemfunga pingu halafu wanamuweka kwenye buti, ni haki kweli? Kwani ni jambazi?!

“Basi, kufika kituoni, wakamtoa na kumwingiza ndani ya kituo. Hali yake ikaonekana kuwa mbaya, maana pia alikuwa akilalamikia maumivu ya mbavu upande wa kulia. Kwa hiyo, tukasema tumpeleke polisi, wao wakasema watampeleka wenyewe.”

“Lakini ndani ya nusu saa, nikamwona kiongozi mmoja wa polisi kutoka ngazi ya mkoa anaingia. Labda aliwasiliana na mtu mwingine yeyote kati yetu.

“Alituita ndani kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo, OC-CID Mwakasungura. Huyo mkuu alimuuliza Mwakasungura kama anawajua askari waliokwenda kwenye tukio, akajibu anawajua lakini akasema shauri lilifunguliwa Wazo Hill. Mkuu yule akamuuliza kama kuna askari wa Wazo hata mmoja aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, akasema hakuna.”

“Yule mkuu akaomba aende hospitali kumwangalia majeruhi, maana wakati huo wale askari walishampeleka Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.”

“Baada ya vipimo vya Ultra Sound na X-ray, ilibainika kuwa, Manyama aliumia mbavu za mkono wa kulia na pia ilibidi ashonwe sehemu ya paji la uso alikochanika. Mwenyewe anasema alipigwa na kitako cha bunduki akachanika na mbavuni alipigwa na mabuti.”

“Baada ya kumwona majeruhi, kiongozi huyo wa polisi aliitisha mkutano mfupi pembeni kidogo, nikiwemo mimi, mkurugenzi wangu, Shigongo, Mwakasungura na wale askari. Kila mmoja alijieleza alivyolijua lile tukio. Mwishowe yule kiongozi akamwagiza Mwakasungura kuchukua maelezo ya askari hao kwa kina na maelezo ya wafanyakazi wa eneo la tukio, kisha yaende kwake.

“Kinachoonekana, walitakiwa wale askari kuwa na hata mmoja wa askari wa Wazo Hill. Lakini pia walitumia nguvu kubwa sana kumkamata Manyama ambaye si mlengwa. Lakini mbaya zaidi, Sophia alipoona mtiti wa pale ofisini alikimbia. Kwa hiyo askari wakawa wanamshika mtu bila mlalamikaji. Waliingizwa chaka na Sophia.”

“Kwa kweli mimi kama raia mwema na Manyama pia ni raia mwema. Wito wangu kwa askari ni kuwa makini sana na oparesheni zao. Nyingi ukiziangalia zina sura ya hisia mbaya. Kama mtu si jambazi anafanyiwa vile, hii si sawasawa. Weledi ni jambo muhimu sana katika kazi zao.”

Kwa mujibu wa RB iliyoandikishwa katika kituo cha Polisi Wazo Hill, Sophia alilalamika kuwa watu wa taasisi ya mikopo walikwenda nyumbani kwake kufanya fujo, jambo ambalo meneja Samson a.k.a Sam alilikanusha vikali.TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright SUKARI GURU
Back To Top