TANGAZO 1
ASP, Thomas Njiku.
IMEFAHAMIKA kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Thomas Njiku (40),
ambaye aliuawa kwenye mapambano na majambazi ana mwezi mmoja tu tangu
ahamishiwe Kanda Maalum ya Dar es Salaam, akitokea mkoani Manyara.
Ilielezwa na vyanzo mbalimbali kuwa Njiku alikuwa Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majambazi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Marehemu Njiku aliuawa alfajiri ya jana eneo
la Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani, wakati akiongoza kikosi
maalum cha kuwasaka watu wanaosadikika kuwa ni majambazi.
Ilielezwa kuwa marehemu pia alikuwa akionekana
mara kadhaa kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam akiongoza
misafara ya ulinzi wa askari waliokuwa wakisindikiza watuhumiwa wa kesi
za ugaidi.
“Kila mara alikuwa akija na msafara
watuhumiwa wa makosa ya ugadi katika kesi ya wakina Sheikh Faridi Hady
Ahmed na wenzake zaidi ya 20,” kilieleza chanzo hicho.
Pia kilielezai kuwa marehemu Njiku alikuwa
akiongoza misafara ya kesi za viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani
kama Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) walipokuwa
wanafikishwa mahakamani kwa kesi mbalimbali.
Chanzo kingine katika Mahakama hiyo kilisema
hadi juzi marehemu alikuwa katika Mahakama hiyo akitekeleza majukumu
yake kabla ya alfajiri ya jana kwenda kwenye tukio hilo lililokatisha
uhai wake.
“Tulikaa naye juzi (Jumatano) tukawa
tunakunywa naye chai hapa Kisutu, tukawa tunapiga porojo za maisha ya
hapa na pale na nakumbuka aliniambia nisilipie chai yangu atalipa yeye,
ni mtu mpole na mcheshi alikuwa rafiki yangu sana,” kilieleza chanzo
hicho.
Mmoja wa askari aliyekuwa akifanya kazi na
Njiku alimwelezea kuwa ni mchapa kazi na hodari kwenye utekelezaji wa
majukumu yake ya kila siku.
“Siwezi kumzungumzia sana marehemu Njiku kwa
sababu nimemfahamu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu tangu ahamishiwe
hapa, lakini alikuwa mchapa kazi na anayejituma sana,” alisema mmoja wa
askai hao, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Namna afande Njiku alivyouawa
Umauti ulimkuta afande Njiku muda mfupi baada
ya vikosi vya Jeshi la Polisi vikiwa na silaha mbalimbali kuwasili
kwenye nyumba hiyo meeneo ya Vikindu.
Njiku ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa msafara
wa vikosi hivyo vya polisi alifariki baada mtuhumiwa anayedaiwa kuwa ni
jambazi kumfyatulia risasi ambazo zilimpata kichwani kusababisha kifo
chake.
Kifo cha afande Njiku kimeongeza idadi ya
askari waliouwawa ndani ya wiki moja pekee kufikia watano baada ya wale
wanne waliouwawa na majambazi Mbande Wilaya ya Temeke.
Njiku aliuawawa mara tu askari hao walipofika
karibu na nyumba hiyo na yeye kuanza kuwapanga vijana wake kwa kutoa
maelekezo ya namna ya kukabiliana na watuhumiwa waliokuwa ndani ya
nyumba hiyo.
“Wakati Njiku akitoa maelekezo kwa polisi
wenzake, inasemekana mtuhumiwa huyo aliyefyatua risasi iliyomuua askari
wetu alikuwa kwenye moja ya madirisha ya nyumba hiyo akiangalia namna
askari hao wanavyojipanga nje ya nyumba hiyo na ndipo akamuua,” alisema.
Chanzo hicho kilieleza kuwa baada ya mtuhumiwa
huyo kupiga risasi hizo zilizosababisha kifo cha askari huyo,
majibizano ya risasi kati ya polisi na watuhumiwa wa ujambazi
waliokuwamo ndani ya nyumba yalipoanza na polisi kufanikisha kuwaua watu
14.
Pia chanzo hicho kilisema kuwa Jeshila Polisi
lilifanikiwa kuwakamata watu watano akiwemo askari mstaafu wa Jeshi la
Wananchi (JWTZ) ambaye alikuwa mtaalamu wa utunguaji (Sniper).
Jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro hakuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusu tukio hilo
na aliahidi kuwa leo ndipo ataweka hadharani kilichotokea huko Vikindu.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment