TANGAZO 1
Rais John Pombe Magufuli kupitia WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye, amemteua Bw. Hassan Abbas, (pichani) kushoto ,
kuwa Mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari Maelezo, akichukua nafasi
iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene ambaye alihamishiwa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Akitangaza uteuzi huo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Agosti 9,
2016, Nauye aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kufuatia uhamisho wa
Bw. Mwambene uliofanyika Machi 7, 2016, ilibidi mchakato wa kujaza
nafasi hiyo uanze na kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya
mwaka 2002 kifungu cha 6(1) na (b) Bw. Abbas ameteuliwa kujaza nafasi
hiyo kuanzia Agosti 5, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abbas ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari,
alikuwa Meneja Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia
utekelezaji wa Program ya Matokeo Makubwa Sasa (Presidential Delivery
Bureu).
Miongoni mwa majukumu ya Mkurugenzi huyo, ni pamoja na kuwa Msemaji Mkuu
wa Serikali na Mkuu wa vitengo vyote vya serikali vinavyoshughulika na
masualaya mawasiliano ya Umma, alisema Waziri Nape.
Akizungumzia uteuzi huo Bw. Abbas alisema, yeye alianza kama mwandishi
wa habari wa kujitegemea (correspondent), ambapo alikuwa kilipwa kwa
habari anayowasilishana kutumika, na kisha kuwa mwandishi wa habari wa
kawaida kabla ya kupandishwa cheo na kuwa mhariri wa habari na baadaye
kuwa kaimu mhariri na kabla ya kupanda cheo na kuwa mhariri kamili.
Waziri Nape alichukua nafasi hiyo kumshukuru aliyekuwa akikaimu nafasi
hiyo, Bi. Zamaradi Kawawa na kumuelezea kuwa aliifanya kazi hiyo kwa
uadilifu na kujituma kwa kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu.
Waziri Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akizungumza
Waziri Nape, Bw. Abbas na Bi. Zamaradi wakisikikliza maswali ya waandishi wa habari
Waandishi wa Habari wakitekeleza majukumu yao
Mkutano ukiendelea
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment