TANGAZO 1
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimeanza
kugawa vifaa zikiwemo bendera kwa ajili maandalazi ya Umoja wa Kupinga
Udikteta ( Ukuta) ambayo yanatarajia kufanyika Septemba mosi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Katibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Casimir Mabina, alisema kuwa
bendera hizo zitaanza kupeperushwa kuanzia kesho kutwa kwa ajili ya
kuunga mkono azimio la Kamati Kuu ya kufanyika oparesheni Ukuta.
Alisema oparesheni Ukuta ni lazima ifanyike nchi nzima na kwamba
hawako tayari kuona ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na
serikali ya awamu ya tano ambayo imeonyesha viashiria vya utawala wa
kidikteta.
Alisema Rais John Magufuli, anajaribu kuua demokrasia ya vyama
vingi kwa kukataza na kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani
huku CCM ikiendelea na mikutano yake kama kawaida.
“Tumeona jinsi Rais alivyopiga marufuku wapinzani kukutana
kwenye mikutano ya hadhara huku akiwatishia kuwa wakikaidi
atawashughulikia na kweli amewaamuru polisi watekeleze amri hiyo ya
kuwakamata viongozi wa Chadema na kuwafungulia mashtaka,” alisema
Aliongezea kuwa mbaya zaidi Jeshi la Polisi linazuia hata mikutano
ya ndani ya vyama vya upinzani na makongamano na hata mahafali ya
wanafunzi wenye itikadi za upinzani licha ya kutambua kuwa mikutano ya
ndani haiwezi kuleta uvunjifu wa amani kwa walio ndani ya ukumbi.
Alisema licha ya kwamba Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli. amekataza
mikutano hiyo kufanyika chama tawala, kinafanya mikutano ya hadhara
katika maeneo mbalimbali kwa kisingizio cha shughuli za serikali.
Mabina alisema juzi CCM ilisema itakuwa na maandamano kutoka uwanja
wa ndege wa Mwalimu Nyerere ya kumpokea Rais Magufuli hadi Makao Makuu
ya CCM yaliyopo Lumumba.
“Tunahoji haki ya kufanya siasa ni kwa CCM tu na siyo kwa vyama
vingine? Hili jambo hatuwezi kukubali Jeshi la Polisi lituambie
inakuwaje vibali vinatolewa kwa CCM halafu upinzani tunyimwe tunasema
lazima tufanye oparesheni Ukuta ya kupinga ukandamizaji wa demokrasia,” alisema Mabina
Naye Katibu wa Wabunge wa Upinzani Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa
Viti Maalum, Anatropia Theonest, alisema lengo la oparesheni ya Ukuta
ni kupinga ukandamizaji unaofanywa na serikali.
Alisema wana haki ya kikatiba ya kufanya mikutano bila kuzuiliwa
kama ambayo wamefanyiwa na ndio maana wameanza kugawa bendera kwa ajili
ya kujiandaa na oparesheni hiyo.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3

Post a Comment