TANGAZO 1
KUHUSU WITO WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUKUTANISHA VYAMA KWA AJILI YA MAZUNGUMZO.Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeusikia wito uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kikao cha mazungumzo .
Katika hatua ya sasa, tungependa kusema yafuatayo kuhusu kauli za Msajili Jaji Mutungi;
1. Tumeusikia wito wake wa kuitisha meza ya majadiliano na mazungumzo ambayo iwapo yatatawaliwa na nia njema na dhamira safi ya kuheshimu Katiba ya Nchi na utekelezaji wa sheria za Nchi bila kupindisha pindisha, hususan Sheria ya Vyama vya Siasa, yanaweza kuwa na manufaa kwa Watanzania wote.
2. Wakati Msajili wa Vyama akitoa kauli ya kuzuia kile anachokiita 'kutunishiana misuli', Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ya nchi limeingilia vikao vya ndani vya CHADEMA na kuzuia visiendelee. Hiyo yote ni kinyume kabisa na sheria, taratibu na mamlaka yao.
3. Mbali na kuzuia vikao vya ndani, Jeshi la Polisi linashikilia watu mbalimbali, wakiwemo wafuasi, mashabiki, wanachama, viongozi wa CHADEMA kwa kushiriki katika vikao hivyo wakitekeleza wajibu na haki zao za kikatiba na kisheria.
4. Wakati tunasubiri meza ya mazungumzo kupitia Baraza la Vyama, tunapenda kusisitiza kuwa CHADEMA itasimama imara kuhakikisha misingi ya demokrasia na utawala unaozingatia katiba na sheria unafuatwa
Aidha tunawataka wananchi wote wapenda amani waendelee na maandalizi ya UKUTA .
Imetolewa leo Jumanne, Agosti 23, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMATANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment