TANGAZO 1
KIGOGO MZITO SHOGA!
Stori: Mwandishi wetu
WAKATI masuala ya ushoga yakipingwa kwa nguvu zote hapa nchini, skendo
ya aina yake imeikumba serikali baada ya siri kuvuja kuwa mmoja wa
viongozi kumi wa juu nchini ni shoga.
Taric Jumbe akitoa ushuhuda jinsi alivyofanya mapenzi na kigogo huyo.
Habari hizo za kushtua na kufedhehesha taifa ambazo zimefanyiwa kazi na
dawati la Ijumaa kwa kushirikiana na kitengo cha OFM cha Global, zilitua
hivi karibuni chumba cha habari kupitia kwa kijana aliyejitokeza na
kueleza alivyofanya mapenzi ya jinsia moja na kigogo huyo ambaye jina
lake linahifadhiwa kwa sasa.
KIJANA HUYO NI NANI?
“Mimi naitwa Taric Jumbe, nina miaka 21, nimefika hapa kutoa ushuhuda
wangu kuwa nilifanya mapenzi na... (anataja jina), tulianza kuchat
kwenye Facebook, akaniomba urafiki, nikamkubalia nikijua ni wa kawaida
tu.
“Baadaye akaanza kunitongoza na kuniahidi fedha nyingi, nikakubali. Siku
ya kwanza tulikutana Dar, Hoteli ya Serena, akanielekeza chumba
alichopo (anataja namba ya chumba), nikaenda na kuwakuta walinzi wake,
nilipojitambulisha wakaniruhusu kuingia chumbani kwake. Nimeshafanya
naye mara tatu,” alisema kijana huyo.
JINSI WALIVYOWASILIANA
Mbali na matumizi ya mtandao wa kijamii, wanahabari wetu walitaka kujua
mpaka kijana huyo anafika hotelini hapo, alikuwa akiwasiliana na kigogo
huyo kwa njia gani? Jumbe akasema:
“Mwanzo nilikuwa nawasiliana naye kwa Facebook lakini tulipozoeana alinipatia namba zake za simu.”
Jibu hilo lilitoa mwanya kwa makachero wa gazeti hili kuperuzi mtandao
wa simu ile ili kujua kama anayeitumia namba hiyo ni kigogo huyo au ni
changa la macho.
Bila chenga ilibainika kuwa namba hiyo ni ya kigogo huyo, lakini
ilipopigwa kwa lengo la kuwasiliana naye moja kwa moja, iliita bila
kupokelewa na kuwafanya waandishi kuendelea na kazi ya kumhoji kijana
huyo kwa kina.
Taric akiwa ndani ya Global kuelezea sakata hilo la kufanya mapenzi na kigogo serikalini.
KUHUSU MALIPO
Jumbe aliweka wazi kuwa siku ya kwanza kukutana naye alilipwa shilingi
elfu themanini sambamba na ahadi kuwa wakati wowote atakapokuwa na shida
awasiliane na kigogo huyo ambaye msafara wake huongozwa na pikipiki
yenye king’ora na gari la polisi, kwa lengo la kuwezeshwa kimaisha.
Aliongeza kuwa kiasi kikubwa alichowahi kuhongwa ni shilingi laki tatu
(300,000), huku akiainisha kwamba fedha nyingine alikuwa akipewa
kidogokidogo kwa ajili ya kujikimu.
MSHANGAO MWINGINE
Mbali na kijana huyo kukiri kufanya mapenzi mara mbili na kigogo huyo
hotelini, mshangao ulikuja pale alipoweka wazi kuwa mara ya tatu
alimfuata kiongozi huyo nyumbani kwake ambako alishirikiana naye tendo
hilo la aibu.
Waandishi walipotaka kujua waliwezaje kufanya uchafu huo nyumbani kwa
kigogo huyo mwenye familia, Jumbe alisema: “Ni kweli anaishi na familia
lakini nje ya nyumba yake ana ofisi, huko ndiko alikonikaribisha na
kunifanyia mchezo huo.”
UPEKUZI WA MAWASILIANO
Baada ya maelezo hayo, waandishi wetu waligeukia uchunguzi wa
mawasiliano ya simu na mtandao wa Facebook baina ya Jumbe na kigogo huyo
ambapo walibaini kuwepo kwa mambo ya aibu kubwa.
Kwa macho maangavu, waandishi wetu walioneshwa meseji alizokuwa akituma
kigogo huyo ambazo chache kati ya hizo zilisomeka: “Baby, mke wangu,
honey,” huku Jumbe naye akichagiza majibu kwa mtindo huohuo hadi naye
kufikia mahali pa kumwita kigogo huyo ‘mume wangu’, aibu iliyoje!
Kama hiyo haitoshi, wawili hao walifikia hatua ya kusifiana namna
walivyoumbika na kupeana mapenzi motomoto na kuahidiana kuwa pamoja
milele. Kufuru kubwa kwa Muumba!
WIVU HAUKUKOSEKANA
Katika hali ya kustaajabisha na kuonesha kuwa kigogo huyo amekubuhu
kwenye mambo hayo, wakati mwingine akiwa nje ya nchi alidiriki kumuonea
wivu kijana huyo ambapo mara kadhaa alituma meseji ya kutishia kumwacha
kutokana na kile alichokiita ‘kutoka nje ya ndoa’.
Moja kati ya meseji hizo za fedheha kutoka kwa mheshimiwa huyo,
ilimtuhumu Jumbe kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine,
jambo ambalo kijana huyo alilikanusha na wote kuwekana sawa kwa lengo la
kusonga mbele na uhusiano wao.
KIGOGO MZITO AHOJIWA
Baada ya kupata maelezo hayo ya kutisha na kusikitisha, kwa zaidi ya
mwezi mzima, gazeti hili lilifanya juhudi za kumtafuta kigogo huyo ili
kuweza kupata maelezo yake kuhusiana na mkasa huo.
Hatimaye, kwa namna ya kijasusi, Ijumaa liliweza kumfikia na kummwagia
data zote, zikiwemo picha za kijana huyo na nakala ya mawasiliano katika
mtandao wa Facebook ambapo alionekana kuduwaa.
Hata hivyo, kutokana na waandishi wetu kufanya mahojiano na kigogo huyo
huku wapambe wake wanaomlinda na kumuongoza wakiwepo, haikuwezekana
kufungua kila kitu wazi kwa vile mazungumzo hayo yalikuwa yakirekodiwa.
Baada ya kuoneshwa tuhuma zake kwa kutumia nyaraka, mheshimiwa huyo
alikiri: “Nazifahamu hizi nyaraka.” Akimaanisha alichokiona kinamhusu
kwa asilimia mia moja.
TAHADHARI
Tunapenda kuutaarifu umma kuwa tumeamua kulificha kwa makusudi jina la
kigogo huyu ili kuilinda heshima yake ambayo ni kubwa katika jamii yetu.
Tutaliweka wazi wakati wowote endapo kati ya mambo haya yatajitokeza.
Mosi, kijana huyo (Jumbe) atadhuriwa. Tunajua nguvu alizonazo mheshimiwa
huyu ni kubwa, tunaomba kumfahamisha kwamba tutamuanika hadharani
endapo Jumbe atafikwa na matatizo yoyote yasiyo ya kawaida.
Pili, endapo tutathibitisha kuwa anaendelea na mchezo wake huu
usiokubalika na mwisho, endapo waandishi waliokwenda kufanya naye
mahojiano, ambao yeye na wapambe wake wanawafahamu, watapata madhara
yoyote.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3

Post a Comment