TANGAZO 1
WAFANYABIASHARA wawili, akiwemo Mohamed Yusufali “Choma”,
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakikabiliwa na mashitaka 222 ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi
ya Sh bilioni 14.
Mbali na Yusufali aliyewahi kutajwa kuwa anajipatia Sh
milioni saba kwa dakika moja kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya
serikali, mshitakiwa mwingine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern
Engineering Works Limited, Samwel Lema, ambao wanadaiwa kusababisha
hasara kwa kughushi na kukwepa kulipa kodi.
Washitakiwa walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa
mashitaka kwa zaidi ya saa tatu na Wakili Mwandamizi wa Serikali,
Mutalemwa Kishenyi, akisaidiwa na Jackline Nyantori, Diana Lukondo na
Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
Leonard Swai.
Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri, ilidaiwa, katika
tarehe tofauti kati ya Januari Mosi 2012 na Desemba 31, 2014,
washitakiwa hao na wengine ambao hawajafikishwa mahakamani walipanga
njama za kuidanganya Mamlaka ya Mapato (TRA) na kujipatia Sh
14,052,011,435.
Wakili Kishenyi akisaidiwa na Nyantori walidai, katika
shitaka la tano hadi 103 kuwa, kati ya mwaka 2011 na 2013, jijini Dar es
Salaam na Arusha, washitakiwa hao walighushi stakabadhi za malipo
kuonesha Kampuni ya Northern Engineering Works Ltd imenunua bidhaa
mbalimbali.
Ilidaiwa kuwa stakabadhi hizo zilionesha kuwa kampuni hiyo
imenunua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye kampuni tofauti tofauti ikiwemo
ya Festive General Business Ltd, Ever Global General Trading na Jambo
Product Ltd, jambo ambalo si kweli.
Wakili Diana na Swai waliendelea kudai, katika shitaka la
104 hadi 141, kuwa kati ya mwaka 2011 na 2015, Lema alighushi hati ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuonesha kuwa kampuni yake imenunua
bidhaa mbalimbali kutoka kampuni tofauti tofauti ikiwemo ununuzi wa
vifaa vya Sh bilioni 1.7.
Wakili Swai alidai katika shitaka la 142 hadi 219 kuwa, kwa
lengo la kufanya udanganyifu washitakiwa hao walighushi stakabadhi za
malipo kuonesha Kampuni ya Elerai Constructions Ltd, imenunua vifaa
mbalimbali kutoka katika kampuni tofauti tofauti ikiwemo Kampuni ya Blue
Arrow Tanzania Ltd.
Aliendelea kudai shitaka la 220, linamkabili Lema ambaye
anadaiwa kati ya Januari Mosi, 2012 na Desemba 31, 2015, Dar es Salaam,
akiwa Mkurugenzi anayehusika kushughulikia Kampuni yake ya Northern
Engineering Works Ltd na Elerai Constructions Ltd zilizosajiliwa kama
walipa kodi, aliwasilisha nyaraka za uongo.
Inadaiwa aliwasilisha nyaraka ambazo ni marejesho ya uongo
ya Kodi ya VAT kwa Kamishna Mkuu wa TRA jambo lililosababisha akwepe
kulipa kodi ya Sh bilioni 14,052,011,435.
Katika mashitaka ya utakatishaji wa fedha, ilidaiwa kati ya
Februari Mosi, 2012 na Februari 25, 2013 jijini Dar es Salaam na
Arusha, washitakiwa hao walijihusisha na kuhamisha Sh milioni 420
zilizotokana na vitendo vya uhalifu.
Inadaiwa waliziingiza fedha hizo kwenye akaunti namba
1010000541 inayomilikiwa na Iqbal Jaferali Jafferjee iliyopo katika
Benki ya I&M tawi la Kariakoo, na kuzitoa huku wakijua zimepatikana
kwa njia za uhalifu ambazo ni kughushi na kukwepa kulipa kodi.
Iliendelea kudaiwa katika shitaka la 222 kuwa, kati ya
Januari Mosi, 2012 na Desemba 31, 2015, Dar es salaam, kutokana na
vitendo vyao vya kuwasilisha marejesho ya VAT ya uongo kwa Kamishna Mkuu
wa TRA waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh bilioni 14.
Hakimu Mashauri aliwaeleza washitakiwa hao kuwa,
hawaruhusiwi kujibu mashitaka yao kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka
ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu.
Baada ya kusomewa mashitaka, upande wa Jamhuri ulidai
upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya
kutajwa, hata hivyo Wakili Alex Mgongolwa anayeongoza jopo la Mawakili
wa Utetezi aliomba kuwasilisha ombi.
Aliiomba Mahakama ifute shitaka la utakatishaji wa fedha
kwa kuwa lina mapungufu makubwa ya kisheria ambayo hayawezi kurekebishwa
wala kufumbiwa macho isipokuwa kufutwa.
Alidai ili shitaka liwe la utakatishaji wa fedha lazima
kuwa na dhamira ya kuficha chanzo cha fedha au lengo la washitakiwa
kukwepa adhabu lakini kama hakuna mambo hayo sheria inatoa mamlaka kwa
Mahakama kuyafuta mashitaka hayo.
Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo ili
wajiandae kujibu hoja za upande wa utetezi. Hakimu Mashauri alikubali
ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kusikiliza
majibu ya Jamhuri.
Washitakiwa wote walirudishwa rumande kwa kuwa mashitaka
yanayowakabili hayana dhamana. Mbali na mashitaka hayo, Choma
anakabiliwa na kesi nyingine yenye mashitaka 199 ya kuisababishia
serikali hasara ya Sh bilioni 15.6 katika mahakama hiyo
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment