TANGAZO 1
Wizara
imepokea taarifa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Shinyanga
imevamia ofisi za shirika la Jhpiego mkoani humo na kukamata baadhi ya
watumishi wake kwa madai ya shirika hilo kugawa mafuta maalumu
yanayodhaniwa kutumiwa kuhamasisha ngono za jinsia moja. Baada ya taarifa hiyo wizara inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
Si
kweli kwamba shirika la Jhpiego limekuwa likihamasisha ngono baina ya
wapenzi wa jinsia moja. Shirika hilo kupitia mradi wa “Sauti” linasaidia
serikali katika jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kwa makundi yaliyopo kwenye hatari kubwa ya maambukizi.
Moja
ya makundi yanayolengwa ni wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao.
Shirika limekua likitoa elimu ya mabadiliko ya tabia kwa wanaume hao
huku likiwapatia mafuta hayo kama sehemu ya kuwasaidia kupunguza hatari
ya maambukizi.
Mafuta
hayo yaliingizwa nchini kwa kufuata taratibu za kisheria kwa ufadhili
wa Mfuko Maalumu wa Rais wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya
virusi vya UKIMWI (PEPFAR).
Ndugu
wanahabari, kama mtakumbuka hivi karibuni Wizara kupitia kwa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
ilisitisha ugawaji wa mafuta hayo maalumu (vilainishi) miongoni mwa
makundi hayo maalumu.
Kufuatia
agizo hilo, Wizara iliagiza Shirika hilo kukusanya mafuta hayo na
kuyarudisha katika ofisi za PEPFAR zilizopo Ubalozi wa Marekani ili
yapelekwe katika nchi nyingine zinazofadhiliwa na PEPFAR ambazo matumizi
ya mafuta hayo hayajazuiwa.
Ndugu
wanahabari, Shirika hilo lilitekeleza agizo la wizara la kukusanya
mafuta hayo na kuyaweka katika ofisi zao za kanda, tayari kuyasafirisha
kuja jijini Dar es Salaam, ambapo umeandaliwa utaratibu maalumu wa
kuyapeleka katika nchi nyingine bila kuyaharibu.
Mnamo
tarehe 27 mwezi July, mwaka 2016 Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani
Shinyanga ilivamia Ofisi za Shirika hilo na kuchukua mafuta hayo bila
kuelewa utaratibu uliotolewa na Wizara wa kukusanya mafuta hayo na
kuyarudisha katika ofisi za PEPFAR.
Zoezi
hilo la kamati ya Ulinzi na Usalama halikushirikisha wizara ya Afya
wala wadau wa sekta ya Afya wilayani humo, ambao wanaelewa vizuri
utaratibu uliowekwa na wizara kukusanya mafuta hayo na kuyarudisha
mahali husika bila kuyaharibu.
Ndugu
wanahabari, tayari Wizara imeshamuandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa
wa Shinyanga kutaka mafuta hayo yaliyochukuliwa kurudishwa katika ofisi
za mradi wa Sauti zilizopo mtaa wa Mwasele, kata ya Kambarage mkoani
Shinyanga ili zoezi la kuyakusanya na kuyarudisha Dar es Salaam liweze
kuendelea.
Mwisho,
Wizara inapenda kuwajulisha kuwa shirika la Jhpiego ni miongoni mwa
wadau wakuu wa Serikali ambao wamekuwa wakisaidia huduma mbalimbali za
Afya nchini ikiwemo kusaidia ujenzi wa vituo vya afya, kupambana na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kuboresha Afya ya mama na mtoto na
Uzazi wa Mpango kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Hivyo serikali imeridhia
shirika hilo kuendelea kutoa huduma mbalimbali za afya bila kutumia
mafuta hayo.
Imetolewa na:
Michael O. John
Kaimu Katibu Mkuu,
Wiza ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoTANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment