TANGAZO 1
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi
amelaani vikali tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari,
kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya
mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la
kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na
Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na
Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c)
inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au
vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.
“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia
vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.
Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye
kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona
ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka
Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.
Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f)
kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia
lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au
ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya
Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza
chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.
Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha
siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu
yoyote au chama cha siasa chochote.
Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).
Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu
wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa
CHADEMA wasiendeleze tabia hii.
Jaji Mutungi ametoa rai kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa
waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika
vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au
kufarakanisha Umma na Serikali yao.
Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi
Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo
maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa
zitahusika.
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment