TANGAZO 1

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya
Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi
wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza
uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi
ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.
“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole
kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni
mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa
naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.
Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza
kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa
moja kupitia luninga.
“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu
hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa
kuwahudumia wananchi.
“Kipindi kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh
bilioni nne, ni vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’
zikapelekwa katika kesi za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu
kusikilizwa hadi kumalizika kwake,” alisema.
Alisema mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka
2015/2016 ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa
hawajapewa.
“Kiongozi lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima,
watu wa mahakama mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano
nitakuwa nimewapa Sh bilioni 12 zote.
“Sina tatizo la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya
mwaka huu nitawapa fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha
zipo,” alisema.
Mahakimu Kutumbuliwa
Rais Magufuli alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu
502 ambao hawakufikia malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka.
Walimaliza kesi chini ya 100.
“Mahakimu ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako
Jaji Mkuu, unatakiwa kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo
unapitisha agizo mwingine anapinga.
“Unatoa siku saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu,
nakuagiza wachukulie hatua, tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.
“Walioshindwa kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata
ukitangaza leo watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia
mahakama,” alisema.
Mabilioni ya NIDA
Akizungumzia hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), alisema ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho
vilivyotengenezwa havifiki hata milioni mbili na havina sahihi wakati
vitambulisho vya kupigia kura fedha iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70,
lakini vina sahihi za wapigakura wote wa Tanzania ambao ni milioni
23,253,982.
“Utaona ugumu wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo
watu wanacheza na fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana,
wengine wanataka bodi zao wakakae Ulaya.
“Hapo ndipo tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni
35, naomba mniombee kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa
wanaotaka kuifikisha nchi pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.
Kesi za Wakwepa kodi
Rais Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa
Serikali ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi
ya sita.
Alimuomba Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo
Sh trilioni moja ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni
750 zilizobakia zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL
waliopo sasa wataondolewa.
Akizungumzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za
watu waliokutwa na nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano
hazijaamuliwa kwa sababu upelelezi bado.
“Polisi wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona
tatizo lilipo, DPP upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.
Alisema suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi
halihitaji kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama
ianze kwani nchi inachezewa.
Pamoja na hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote
yaliyotolewa na mahakama na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono
ikiwamo kukubali watumishi wa Idara ya Mahakama wasome na kupatiwa
mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
“Nimeamua nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama
yeye, nategemea zaidi mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.
TANGAZO 2
KUTIZAMA PICHA ZAKE NA VIDEO ZAKE ALIZO PIGA AKIWA UCHI NI RAHISI BONYZA HPA CH1NI
TANGAZO 3
Post a Comment